Leo katika mapishi hapa Njoo Tupike , twajifunza jinsi ya kumwandaa kuku wa kuchoma kwa oven ( na sio lazima kwa oven hata kwa jiko la kawaida) cha muhimu ni yale maandalizi ( marination)
MAHITAJI
- Vegetable oil
- Vitunguu swaumu
- Kitunguu maji kimoja kidogo / kipande tu
- chumvi
- Dried Oregano
- Tangawizi
- Pilipili
- Chicken Masala ( Ila mimi katika mapishi yengu ninayo masala special ila wewe waeza tumia aina yoyote)
Kwanza kabisa andaa viungo vyako vya kumuanda kuu.. Twanga tangawizi, kitunguu swaumu, na chumvi kwa pamoja vilainike kabisa. Kisha weka huo mchanganyiko katika bakuli na ongeza kiasi kidogo cha Oregano ( dried oregano, korogoa kisha ongeza vegetable oil na koroga, weka ile chicken masala tayari pia.
Sasa mwanda kuku wako kwa kumuosha vizuri na kisha mimina vile viungo na ile chicken masala mchanganye kwa dakika chache kisha iache kwa muda wa dakika 15-30 au zaidi yategemea kama uko na muda. Kwani unapomwacha kwa muda zaidi ile marination yako inaingia vizuri katika kuku wako
Baada ya muda huo basi waweza anza kumchoma kuku wako kwa moto wa taratibu kwa muda usiopungua dakika 45 . Amini nakwambia hapo kuku atakua mtamu.
0 comments:
Post a Comment