Thursday, September 4, 2014


Naam leo nakuonyesha njia rahisi sana ya kutengeneza biskuti nzuri na tamu sana kwa kutumia mahitaji matatu tu. Ni pishi rahisi sana na waweza kutumia jiko la oven au jiko la mkaa wa kawaida.
MAHITAJI
  • Mafuta ya Butter au Blue Band kiasi ya robo kg
  • Sukari ile laini robo
  • Na Unga wa baking (All purpose flour)
NAMNA YA KUANDAA NA KUOKA BISKUTI
Kwanza changanya butter/blueband na sukari – vichanganye hadi vilaini kabisaaa, kisha ongeza unga wa baking hapo pia changanya sana vya kutosha hadi unga uwe washikana – kumbuka mahitaji ni hayo matatu usiongeze maji. Baada ya kuwa umeuchanganya vema unga wako uhifadhi kwa friji au mahali tulivu kwa dakika 20 hivi. Pasha jiko lako moto kama watumia oven au kama ni mkaa uwe tayari.
Baada ya hapo toa na ukande upya kisha tengeneza katika shape za biskuti unazozipenda. Weka katika baking sheet kwa wanaotumia oven – weka katika oven biskuti zako – usiwe mbali na jiko kwani ndani ya dakika 15 – 20 zinatakuwa tayari pale utakapoona zinaanza kuwa brown katika kona na biskuti. Zikiwa tayari wazitoa na kuacha zipoe kwa dakika 5 basi hapo zipo tayari
how to make biscuits with just three ingredients
KWA WATAKAO TUMIA MKAA
Uwe na sufuria kubwa alafu punguza mkaa kabisa katika jiko ikiwezekana acha kijikaa kimoja kidogo sawa – panga biskuti zako katika sufuri weka jikoni kisha funika na palililia mkaa mwingine kwa juu. Uwe makini sana kwa hii kwani ni rahisi kuunguza – ila ukipatia ni njia rahisi sana pia. Uwe unafunua kuchungulia kila baada ya dakika 5.
Waka

Share this:

0 comments:

Post a Comment