Burger Tamu

Test our burger.

Viazi vya kuponda

Simple but health food.

Choma Choma

We have variety of choma style.

Mlo ChapChap

Chapchap food Style.

Thursday, September 4, 2014

jinsi ya kuandaa kuku na kumchoma

 
Leo katika mapishi hapa Njoo Tupike , twajifunza jinsi ya kumwandaa kuku wa kuchoma kwa oven ( na sio lazima kwa oven hata kwa jiko la kawaida) cha muhimu ni yale maandalizi ( marination)
MAHITAJI
  • Vegetable oil
  • Vitunguu swaumu
  • Kitunguu maji kimoja kidogo / kipande tu
  • chumvi
  • Dried Oregano
  • Tangawizi
  • Pilipili
  • Chicken Masala ( Ila mimi katika mapishi yengu ninayo masala special ila wewe waeza tumia aina yoyote)
JINSI YA KUMUANDAA NA KUCHOMA
Kwanza kabisa andaa viungo vyako vya kumuanda kuu.. Twanga tangawizi, kitunguu swaumu, na chumvi kwa pamoja vilainike kabisa. Kisha weka huo mchanganyiko katika bakuli na ongeza kiasi kidogo cha Oregano ( dried oregano, korogoa kisha ongeza vegetable oil na koroga, weka ile chicken masala tayari pia.
Sasa mwanda kuku wako kwa kumuosha vizuri na kisha mimina vile viungo na ile chicken masala mchanganye kwa dakika chache kisha iache kwa muda wa dakika 15-30 au zaidi yategemea kama uko na muda. Kwani unapomwacha kwa muda zaidi ile marination yako inaingia vizuri katika kuku wako

Baada ya muda huo basi waweza anza kumchoma kuku wako kwa moto wa taratibu kwa muda usiopungua dakika 45 . Amini nakwambia hapo kuku atakua mtamu.

Naam leo nakuonyesha njia rahisi sana ya kutengeneza biskuti nzuri na tamu sana kwa kutumia mahitaji matatu tu. Ni pishi rahisi sana na waweza kutumia jiko la oven au jiko la mkaa wa kawaida.
MAHITAJI
  • Mafuta ya Butter au Blue Band kiasi ya robo kg
  • Sukari ile laini robo
  • Na Unga wa baking (All purpose flour)
NAMNA YA KUANDAA NA KUOKA BISKUTI
Kwanza changanya butter/blueband na sukari – vichanganye hadi vilaini kabisaaa, kisha ongeza unga wa baking hapo pia changanya sana vya kutosha hadi unga uwe washikana – kumbuka mahitaji ni hayo matatu usiongeze maji. Baada ya kuwa umeuchanganya vema unga wako uhifadhi kwa friji au mahali tulivu kwa dakika 20 hivi. Pasha jiko lako moto kama watumia oven au kama ni mkaa uwe tayari.
Baada ya hapo toa na ukande upya kisha tengeneza katika shape za biskuti unazozipenda. Weka katika baking sheet kwa wanaotumia oven – weka katika oven biskuti zako – usiwe mbali na jiko kwani ndani ya dakika 15 – 20 zinatakuwa tayari pale utakapoona zinaanza kuwa brown katika kona na biskuti. Zikiwa tayari wazitoa na kuacha zipoe kwa dakika 5 basi hapo zipo tayari
how to make biscuits with just three ingredients
KWA WATAKAO TUMIA MKAA
Uwe na sufuria kubwa alafu punguza mkaa kabisa katika jiko ikiwezekana acha kijikaa kimoja kidogo sawa – panga biskuti zako katika sufuri weka jikoni kisha funika na palililia mkaa mwingine kwa juu. Uwe makini sana kwa hii kwani ni rahisi kuunguza – ila ukipatia ni njia rahisi sana pia. Uwe unafunua kuchungulia kila baada ya dakika 5.
Waka

Share this:




MAHITAJI
  • Nyama robo
  • Ndizi mzuzu mbichi 5
  • Vitungu maji na swaumu
  • Giligilani vijani vichache
  • Rosemary vijani vichache
  • Bay vijani vichache
  • Chumvi
  • Olive oil kijiko cha mezani kimoja
  • Chills – kama watumia
  • Karoti moja
  • Black pepper
KUPIKA
Kwanza chemsha nyama – sasa wakati wachemsha nyama weka chumvi, bay, rosemary, garlic na blackpaper. Ichemke hadi kuiva ndipo uweke vitunguu maji na swaumu pamoja na ndizi kisha acha viive dakika kabla ya kuepua weka karoti.. #enjoy #kudimbadimba
Najua tumezoa yale mapishi ya ndizi nyama, ni vema ujaribu pishi hili la samaki – yaani prawns na king fish-  Ni pishi tamu sana na rahisi sana kulipika.

 

MAHITAJI
  • Ndizi
  • Prawns
  • KingFish
  • Vitunguu Maji na swaumu
  • Rosemary leaves
  • Bay leaves
  • Nazi tui moja zito
  • Black pepper
  • Chumvi
  • Olive Oil
  • Chill flakes (kwa watumiaji pilipili)
KUPIKA
Anza kuchemsha ndizi weka na mafuta, chumvi, bay, rosemary, black pepper, kitunguu swaumu… Wacha zichemke ziive. Ndipo uweke vitunguu Maji , praws, king fish kisha chemsha kwa dakika 3 ndipo uweke tui la nazi na endelea kukoroga lisikatike. Baada ya hapo jipakulie ujinome…. Plz picha hii and share with me. #kudimbadimba